Jinsi ya kupika kaukau za ngano

Na Lucy Samson
14 Sept 2026
kaukauu za ngano, mkombozi wa wapishi jikoni pale wanapopatwa na dharura. Leo Jiko Point tupo hapa tuandae pamoja hatua kwa hatua.
article
  • Kaukau ni miongoni mwa vitafunwa rahisi vya kuandaa nyumbani ndani ya dakika 10 tu.

Unazijua zile nyakati unazotembelewa na ugeni mzito alafu ukitazama ndani hakuna vinywaji wala vitafunwa vya kuwapa wageni?

Katika nyakati kama hizo nafikiri ndipo watu wengi hukimbilia kwa mangi kuagiza soda na biskuti au kuwakalisha wageni na njaa muda mrefu wakati wakiandaa mlo mkuu.

Vipi nikikwambia kuwa unaweza kuandaa vitafunwa rahisi ndani ya dakika 10 tu na kufurahia pamoja na wageni au na familia.

Ndio! pishi hilo ni kaukauu za ngano, mkombozi wa wapishi jikoni pale wanapopatwa na dharura. Leo Jiko Point tupo hapa tuandae pamoja hatua kwa hatua.

Mahitaji

Unga wa ngano

Chumvi

Maji

Mafuta ya kukaanga

Unaweza kla kaukau za ngano pamoja na sosi au pilipili yoyote. Picha| Toast/Facebook.

Maandalizi

Hatua za awali za mapishi ya kaukau zinafanana na zile za mapishi ya chapati hivyo tuanze kwa kuandaa mahitaji yote niliyoorodhesha hapo juu, kisha anza kuchekecha unga.

Lengo la kuchekesha ni kuondoa uchafu na vijidudu vinavyotokana na unga kukaa dukani muda mrefu.

Baada ya hapo weka unga katika bakuli kisha uongeze chumvi kiasi na  maji ya uvuguvugu taratibu na ukande mpaka uwe laini.

Ukiwa laini paka mafuta kiasi kwa juu na uanze kukata madonge madogo kisha uyasukume kutengeneza duara lenye ukubwa kiasi.

Kupitia hilo duara naweza kutenegeneza shepu yoyote unayoipenda kisha bila kupoteza muda choma shepu zako za ngano katika mafuta yaliyopata moto kiasi.

Zigeuze geuze hadi zitakapopata rangi ya kahawia, ziepue na uziache zipoe kisha zitakuwa tayari kwa kula.

© Copyright 2021 JikoPoint by Nukta Africa